Tel: 061 261 57 67
Warenkorb
Ihr Warenkorb ist leer.
Gesamt
0,00 CHF

Siri sirini - Kitabu cha 1

Angebote / Angebote:

Siri imekuwa siri, na si siri tu, bali ni kilinge, yaani kunga. Matesa ametekwa na kufanywa mfungwa. Swali ni: Je, mwanadamu akumbanapo na masuala magumu kama vile amani, uonevu, watawala dhalimu, mapenzi changamano, afanyeje? Atakayemwokoa mwenye kuteseka hajulikani, ni Kidhabi ama ni Mwanalemba? Ni kitu gani kilichomfanya mtetezi kufanywa mhanga, mwinda kuwa mwindwa? Kwa hali yoyote ile, Siri Sirini ni fumbo pevu, lakini upo mwanya mmoja wenye kutufumbulia fumbo lenyewe. Mwanya wenyewe umo kwenye mshororo mmoja baina ya mingine katika shairi, mshororo uliöchama siri kali. Je, siri hii ni siri gani yenye kula vichwa vya wajinga na weledi? Haitanzuki siri, imetanza mba, imekukutaa na ukakamavu! Vikao vya kumfuma "msaliti, " vimeshamiri, vilinge vimekolea, urazini umepotea. Siri, imo sirini! Ni siri gani hii jamani? Siri Sirini: Mshairi na Mfungwa ni riwaya ya kwanza katika msururu wa riwaya tatu zenye ku¿kirisha, kuhifadhi historia kama tarikhi huku masuala ya utawala wa kisiasa na utendajikazi unaotarajiwa katika muktadha huo ukichimuza. Ni riwaya inayosheheni uchangamfu na karipio kwa wakati mmoja. Usomapo riwaya hii ya kwanza, utajikuta umepata hamu kuu ya kuipata ya pili nayo uisome bila kuchelewa, na ukiisoma ya pili, basi hutakuwa na budi bali kuisaka na kuisoma ya tatu vile vile. Rocha Muzungu Chimerah ni mwandishi wa riwaya mwenye tajiriba na kipawa cha aina yake. Anatumia mtindo wa kuchangamsha moto mmoja katika uandishi wake huku akiangazia masuala mazito ambayo wengi hushindwa kupata ujasiri wa kuyaandikia. Ukweli katika mambo yamshughulishayo katika msururu huu wa riwaya ni kama kijembe cha sumu, lakini anavyousema ukweli huo ni kama uki wa nyuki, unaokuacha ukijirambaramba mdomo kitambo kizima baada ya kuumeza uki huo.
Folgt in ca. 10 Arbeitstagen

Preis

40,50 CHF