Tel: 061 261 57 67
Warenkorb
Ihr Warenkorb ist leer.
Gesamt
0,00 CHF

Janga la Werevu

Angebote / Angebote:

Anaingia Mwendawazimu. Kavaa mararu. Kurunzi inamfuata kila anapopiga hatua. Anaonekana mchafu. Hajakoga milele. Kwa hivyo weusi wake wa ngozi umekuwa tititi na kurembwa na weupe wa chumvi ya jasho inayolala juu ya mwili wake siku zote. Anapofika mbele ya hadhira anabingiriabingiria na kugaragara huku akichekacheka kiwazimuwazimu. Kisha anasita ghafla na kutazama mara kadha juu, chini, mbele na nyuma kwa macho yake makali yanayotisha. Anaonekana kama anatafuta kitu au ameona kitu cha ajabu. Hatimaye anaijongelea hadhira na kuikumbusha ...
Folgt in ca. 15 Arbeitstagen

Preis

28,90 CHF